Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na hasimu wake mkubwa Riek Machar walikubaliana Jumatano ya tarehe 27 mwezi Juni mwaka huu mjini Khartoum nchini Sudan, kusitisha kabisa mapigano, hivyo kuongeza matumaini ya kuvifikisha mwisho vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa kipindi cha miaka minne na nusu.