Matangazo
Israel na wanamgambo wa Palestina walitangaza kusitisha mashambulizi Ijumaa usiku wakilenga kuumaliza mgogoro mbaya zaidi kuwahi kutokea kati yao ndani ya miaka saba iliyopita. Makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Misri yamejiri baada ya shinikizo na miito ya kimataifa kutaka machafuko hayo ambayo yamedumu kwa siku 11 kusitishwa. Zaidi kuhusu hatua hii na iwapo itakuwa na manufaa yoyote, Lilian Mtono amezungumza na machambuzi wa masuala ya siasa aliyeko London, Uingereza Ahmed Rajab.