Makumbusho ya maafa Rwanda yaongezwa katika Turathi za Dunia
20 Septemba 2023Matangazo
UNESCO limeandika kwenye mtandao wa X kwamba makumbusho hayo ni ya Nyamata, Murambi, Gisozi na Bisesero na yanayobeba kumbukumbu ya mauaji ya karibu Watutsi 800,000 pamoja na Wahutu waliokuwa na misimamo ya wastani kati ya mwezi Aprili na Julai 1994.
Makumbusho hayo yamesheheni mafuvu ya vichwa, vipande vya mifupa, nguo zilizochanika na picha za maiti zlizorundikana zimekuwa zikiibua hisia kali kwa wageni wanaotembelea makumbusho ya Gisozi, mjini Kigali ambako kulihifadhiwa wahanga wa karibu 250,000 wa mwisho wa mauaji hayo ya kimbari.