Makundi hasimu nchini Haiti yatia saini makubaliano ya amani
26 Julai 2024Haya ni kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa kijamii mwenye ushawishi, kasisi Jean Enock Joseph.
Kasisi Joseph, amesema chini ya makubaliano kati ya viongozi wa vikundi vya G9 na G-Pep, vizuizi vya barabarani katika mtaa huo wa mabanda wa Sun City wenye takriban wakaazi 300,000 viliondolewa.
Polisi wa Kenya wanashika doria katika mji mkuu wa Haiti baada ya vikosi zaidi kuwasili
Kasisi huyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hatua mpya imefikiwa. Hata hivyo ameongeza kuwa makubaliano kama hayo yalitiwa saini mnamo Julai mwaka 2023 kabla ya kusambaratika wiki chache baadaye.
Magenge ya G9 na G-Pep hayajapigana tangu mwezi Februari, walipoingia kwenye muungano.
Hapo jana, Jimmy Cherizier, kwa jina maarufu "Barbecue" kiongozi wa G9 na mmoja wa viongozi wa muungano huo, alisifu "ujasiri" wa viongozi wa genge la Sun City.