1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Palestina yawakamata wafuasi makundi ya itikadi kali

17 Julai 2023

Kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Islamic Jihad limesema kuwa vikosi vya usalama vya Palestina vimewazuilia wanachama wake watano zaidi usiku kucha katika mji wa Jenin hatua walioitaja imeonesha mpasuko.

https://p.dw.com/p/4U0el
Palestina Gefängnis
Picha: Mohammed Abed/AFP/Getty Images

Kundi hilo limesema mpasuko unashuhudiwa zaidi kati ya makundi katika ukingo wa Magharibi wiki mbili tangu Israel ilipofanya uvamizi wake mkubwa katika eneo hilo baada ya miaka kadhaa. 

Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka Israel kuhusu ripoti ya kukamatwa kwa wanamgambo hao ama kutoka kwa vikosi vya ulinzi vya Mamlaka ya  Palestina, iliyo na utawala mdogo katika baadhi ya maeneo ya Ukingo huo wa Magharibi.

Soma pia:Rais wa Mamlaka ya Palestina Abbas azuru mji wa Jenin

Israel, ambayo inasema uvamizi wake wa mwezi huu uliouwa Wapalestina kadhaa uliwalenga wanamgambo kama hao, inaishinikiza Mamlaka ya Palestina kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya makundi ya itikadi kalina Hamas yanayoungwa mkono na Iran na yanayothibiti Ukanda wa Gaza na pia yenye wapiganaji katika Ukingo wa Magharibi.