Malawi yaanza zoezi la chanjo baada ya janga la kimbunga
15 Mei 2023Matangazo
Kulingana na rais wa Malawi Lazarus Chakwera, Kimbunga Freddy kiliua zaidi ya watu 1,000 katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.
Kimbunga hicho kilikuwa moja ya dhoruba mbaya kuwahi kulikumba bara Afrika katika miaka ya hivi karibuni. Mataifa ya Malawi, Msumbiji na Madagascar yaliathirika na kimbunga hicho mwishoni mwa mwezi Februari na Machi.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, lile la Umoja wa Mataifa la kushughulikia watoto UNICEF na muungano wa chanjo wa GAVI, zoezi hilo la chanjo la wiki moja linawalenga watoto wa hadi umri wa miaka 15 na linakusudia kutoa chanjo dhidi ya surua, kipindupindu, rubela na ugonjwa wa kupooza, Polio.