1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMalaysia

Malaysia yajindaa kwa mazungumzo na China kuhusu bahari

3 Aprili 2023

Malaysia inajiandaa kuingia kwenye mazungumzo na China kuhusu mvutano uliopo kati yake katika eneo la bahari ya Kusini mwa China.

https://p.dw.com/p/4PcqA
USS Nimitz Drill Südchinesisches Meer
Picha: ABACA/picture alliance

Hayo yameelezwa leo na kituo cha habari cha taifa ambacho kimemnukuu waziri mkuu wa nchi hiyo Anwar Ibrahim.

Suala hilo lilizushwa kwenye mkutano kati ya waziri mkuu huyo na rais wa China Xi Jinping wiki iliyopita,katika wakati ambapo Malaysia imeanzisha mradi wa kutafiti uchimbaji mafuta na gesi katika eneo hilo.

Waziri mkuu wa Malaysia amesema China nayo inadai eneo hilo ni milki yake na nchi yake ndogo inahitaji mafuta na gesi na kwa hivyo inabidi iendelee na mradi huo. Lakini ikiwa sharti la kufanya hivyo ni kuwepo mazungumzo basi nchi yake iko tayari.

China inadai kuwa na haki ya umiliki wa takriban eneo zima la bahari ya kusini ya China ambalo pia linazozaniwa na Brunei, Ufilipino, Taiwan na Vietnam.