SiasaSudan Kusini
Malori ya msaada wa kibinadamu yakwama kwenye mpaka wa Sudan
25 Aprili 2024Matangazo
Wiki hii, wizara ya biashara nchini humo ilianzisha ushuru mpya wa dola 300 kwa kila lori linalosafirisha bidhaa ndani au nje ya nchi hiyo inapotafuta kuongeza mapato.
UNMISS imesema kutokana na hatua hiyo, serikali ilikuwa bado haijatoa kibali cha kuvuka kwa malori hayo yaliokodishwa na Umoja huo wa Mataifa yaliyokuwa yamepakia mafuta kutoka nje licha ya kuhakikishiwa kuwa yamesamehewa kulipa kodi.
Kaimu msemaji wa UNMISS Priyanka Chowdhury, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanaendelea kufanya mashauriano na maafisa wa ngazi za juu ili kutatua suala hilo.
Misheni za kidiplomasia zimepinga hatua hiyo, huku zikitoa wito wa kuondolewa kwa ushuru huo dhidi ya mashirika ya kibinadamu.