MigogoroHaiti
Watetezi wa haki waiomba Marekani kutowarudisha Wahaiti
28 Machi 2024Matangazo
Shirika lisilo la kiserikali la Haitian Bridge Alliance, lenye makao yake San Diego, hapo jana lilichapisha barua pamoja na mashirika mengine 481 yakiitaka Marekani kuongeza hali ya ulinzi wa muda kwa Wahaiti, isitishe kuwarudisha nchini mwao kwa lazima, iwaachie wahamiaji waliokamatwa na kutanua mipango ya kuwasamehe wakimbizi.
Nchi kama Marekani, Canada na Ufaransa zimekuwa zikiwaondoa raia wao na wafanyakazi wa mashirika kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF kutoka nchini humo.
Mataifa jirani ya Haiti kwa upande wao yamekuwa yakiongeza ulinzi katika mipaka yao na kuwarejesha nyumbani Wahaiti wanaokimbia machafuko, hatua ambayo imelaaniwa na Umoja wa Mataifa.