SiasaTunisia
Mamia ya watu wafanya maandamano nchini Tunisia
12 Mei 2024Matangazo
Imed Khemiri, afisa mwandamizi katika chama cha Ennahda ambacho ni mshirika wa chama cha Salvation Front kinachoandaa maandamano hayo, amesema kuwa kwa sasa hakuna mazingira ya uchaguzi wa haki na pia hakuna tarehe iliyopangwa ya kufanyika kwa uchaguzi huo huku mamlaka ikiwakandamiza wanasiasa, wanasheria na waandishi habari.
Changamoto zinazoikabili Tunisia
Maandamano hayo yanakuja huku kukiwa na mzozo wakiuchumi na kisiasa na wimbi la kukamatwa kwa wanahabari, wanasheria, wanaharakati na wapinzani nchini humo.
Hapo jana, polisi nchini humo walivamia jengo la mawakili na kumkamata Sonia Dahmani, wakili anayejulikana kwa ukosoaji wake mkali wa Rais Kais Saied. Waandishi wawili wa habari pia walikamatwa siku hiyo hiyo.