Mamilioni wajitokeza Iran kumuaga Rais Ebrahim Raisi
22 Mei 2024Matangazo
Televisheni ya taifa nchini humo, ilimuonesha kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, akiongoza ibada hiyo mbele ya majeneza ya Raisi na wenzake wanane walioangamia katika ajali hiyo, akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri hiyo ya kiilsamu Hossein Amir-abdollahian.
Waombolezaji waliokusanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Tehran waliondoka wakibeba majeneza hayo hadi katika uwanja wa uhuru. Rais Ebrahim Raisi atazikwa kesho alhamisi katika mji alikozaliwa wa Mashad karibu na kaburi la Imam Reza, ambaye ni Imamu wa nane wa dhehebu la kiislamu la kishia.
Tayari viongozi mbali mbali wa dunia kutoka India, Jordan Qatar Kuwait, Afghanistan, Uturuki na Iraq wamefika nchini humo kuhudhuria maziko hayo hapo kesho.