1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Mamilioni ya watu wapambana na ongezeko la Joto duniani

16 Julai 2023

Mamilioni ya watu wanapambana na ongezeko la joto duniani leo Jumapili, wakati utabiri wa hali ya hewa ukionyesha kuwepo kwa kiwango cha juu zaidi cha joto nchini Marekani, Ulaya na bara Asia.

https://p.dw.com/p/4TxtO
Hitze in Frankreich
Picha: Gerard Bottino/SOPA Images via ZUMA Press Wire/picture alliance

Kulingana na taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa ya Marekani iliyotangaza mwisho wa juma, imesema mchana unatarajiwa kuwa na nyuzi joto 10 hadi 20 zaidi ya kiwango cha kawaida hasa kwa upande wa magharibi wa taifa hilo.

Soma pia: Wanaharakati wataka walemavu walindwe dhidi ya joto kali

Barani Ulaya, Italia inatarajiwa kufikia kiwango cha juu cha joto cha kihistoria ambapo wizara ya afya imetoa tahadhari kwa miji 16 ikiwemo Rome, Bologna na Florence. Mjini Roma, joto linatarajiwa kufikia nyuzi joto40 kwa Jumatatu na nyuzi joto 43 siku ya Jumanne.

Nayo Japan imetoa tahadhari ya watu kuwa katika hatari ya kupata kiharusi cha joto kutokana na joto kali.

Kituo cha televisheni ya taifa nchini humo kimewapa angalizo watazamaji kuwa joto liko katika kiwango kinachotishia maisha wakati joto likifikia nyuzi joto 40 katika baadhi ya maeneo ukiwemo mji wa Tokyo.