1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man United yaitumbukiza gizani zaidi Everton

27 Novemba 2023

Mashabiki wa klabu ya Everton walifanya maandamano kabla ya mechi yao ya ligi kuu Jumapili dhidi ya Manchester United, kupinga hatua ya Ligi Kuu nchini humo kuwaadhibu kwa kuwaondolea pointi kumi.

https://p.dw.com/p/4ZUbS
Champions League Fußballspiel Manchester Utd - FC Kopenhagen
wachezaji wa Manchester United wakimpongeza mlinda lango wao Andre OnanaPicha: PAUL ELLIS/AFP

Hatua hiyo ilitokana na Everton kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za matumizi ya fedha katika masuala ya kuwanunua wachezaji. Klabu hiyo imekata rufaa kutokana na uamuzi huo wa ligi kuu na wanasubiri uamuzi kuhusiana na hiyo rufaa yao.

Na sasa baada ya mechi ya jana ambapo walifungwa 3-0 na Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani Goodison Park, kocha wa hao the Toffees Sean Dyche alisema kwa sasa, hakuna wanaloweza kufanya ila kukubali matokeo na kusonga mbele.

"Tazama, tunaweza kulia na kusema tumeonewa ambapo ni jambo ambalo sote tunafikiri ni hivyo na nafikiri kila mmoja anafikiri ni hivyo ila ukweli ni kwamba, adhabu tumeshapewa. Kwa hiyo tupambane nayo, unajua mimi si mtu wa kulia lia, hili lishatokea labda rufaa iamuliwe vinginevyo, wacha tuone litakalotokea. Ila hatuezi kuhakikisha chochote. Bila shaka nimewaambia wachezaji, tunachoweza kukihakikisha kwa sasa ni kinachotokea kwa sasa na tunachoweza kufanya," alisema Dyche.

Kwa sasa everton wanaishikilia nafasi ya 19 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wakiwa na pointi 4 tu.

Vyanzo: AP/Reuters