1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroCuba

Meli nne za kivita za Urusi kuwasili Havana wiki ijayo

7 Juni 2024

Cuba imetangaza siku ya Alhamisi kwamba meli nne za kivita za Urusi pamoja na manowari za kijeshi zitawasili mjini Havana wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4gl36
Urusi | Siku ya Jeshi la Maji la Urusi
Meli za kivita za urusi kama zinavyoonekana pichani wakati wa gwaride ya meli hizo katika Siku ya Jeshi la Maji nchini Urusi, Julai 30, 2023Picha: Alexander Kazakov/Kremlin Pool/ZUMAPRESS/picture alliance

Maafisa wa Cuba wamesema hatua hiyo inatokana na "mahusiano ya kirafiki ya kihistoria" kati ya mataifa hayo mawili, huku mvutano ukiongezeka juu ya msaada wa kijeshi wa Magharibi kwa Ukraine katika vita vyake na Urusi.

Wizara ya mambo ya nje ya Cuba imesema meli hizo zitakuwepo Havana kati ya Juni 12 na Juni 17, na hakuna meli yoyote iliyobeba silaha za nyuklia, na kwa maana hiyo hazileti kitisho dhidi ya ukanda huo.

Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya maafisa wa Marekani kusema wamekuwa wakifuatilia meli za kivita za Urusi na ndege zilizotarajiwa kwenda Caribbean kwa ajili ya luteka za kijeshi.