1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika Kusini

Manusura zaidi wapatikana mkasa wa kuanguka jengo Cape Town

8 Mei 2024

Vikosi vya Uokoaji nchini Afrika Kusini vimefanikiwa kuwapata manusura zaidi wa mkasa wa kuporomoka kwa jengo la ghorofa uliotokea siku ya Jumatatu kwenye mji wa mwambao wa Cape Town.

https://p.dw.com/p/4fblo
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametuma salamu za rambirambi baada ya watu 7 kufa jengo la ghorofa lilipoanguka mjini Cape Town.Picha: Rodger Bosch/AFP/Getty Images

Hadi jana jioni jumla ya watu 26 waliokuwa wamenasa kwenye jengo hilo wameokolewa huku idadi ya waliopoteza maisha imefikia watu 7. Juhudi bado zinafanyika ikiwemo kupekua vifusi kwa matumaini ya kuwapata watu zaidi wakiwa hai.

Inaaminika watu 42 bado wamenaswa kwenye vifusi vya zege na chuma. Wakoaji wanasema wamefanikiwa kuwasiliana na angalau watu 11 waliokwama kwenye kifusi na wana imani watawafikia na kuwaokoa.

Kwa jumla kulikuwa na mafundi 75 waliokuwa wakifanya kazi ya ujenzi wakati jengo hilo la roshani lilipoporomoka.Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wale waliopoteza jamaa zao kwenye mkasa huo.