1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Kifo cha mwanamuziki maarufu nchini Ethiopia

3 Julai 2020

Hali nchini Ethiopia imekuwa ya mvutano mkubwa kwa miezi kadhaa. Mambo yanaweza kulipuka baada ya kuuawa kwa mwanamuziki maarufu wiki iliyopita. Haya ni maoni ya mkuu wa matangazao ya lugha za Kiafrika DW, Claus Stäcker.

https://p.dw.com/p/3ekkD
Äthiopien Hachalu Hundessa, ermordeter Künstler
Picha: Leisa Amanuel

Mwanamuziki huyo aliyeuawa Hachalu Hundessa hakuwa kama mtu mwengine yeyote. Kijana huyo aliimba nyimbo za kikabila kwa ajili ya harakati za watu wa kabila la Oromo ambazo zinazidi kuimarika.

Watu wa kabila hilo kihistoria wanaona kuwa wanakandamizwa. Hawakuwamo miongoni mwa wafalme wa kiamharic, madikteta wa kikomunisti na wala hawakuwamo miongoni mwa vyama vya kisiasa vilivyotokana na muungano wa makabila mengi. Nyimbo za Hachalu zinawasislisha ujumbe wa utambulisho, lakini kwa chini chini zinatilia mashaka umoja wa kitaifa.

Serikali kuu na zile za majimbo zinatiliana mashaka kwa kiwango kikubwa

Tangu mwaka 1995 mfumo wa shirikisho nchini Ethiopia, kikatiba umejengwa katika msingi wa makabila. Na tangu kuondolewa kwa utawala wa mkono wa chuma, na tangu kuingia madarakani kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, mivutano ya kikabila imeongezeka.

USA| Protest nach Tod von äthiopischem Sänger und Aktivisten Hachalu Hundessa
Waandamanaji wanaopinga mauaji ya HachaluPicha: Getty Images/S. Maturen

Serikali kuu na zile za majimbo zinatiliana mashaka kwa kiwango kikubwa. Abiy Ahmed aliyeingia madarakani miaka miwili iliyopita sasa yuko chini ya shinikizo kubwa. Yeye mwenyewe anatoka kwenye kabila la Oromo, lakini wanaomuunga mkono wanazidi kupungua. Kwa mujibu wa taarifa, ni watu wa kabila la Amharik tu wanaomuunga mkono katika nchi ya Ethiopia yenye majimbo 80. Hata hivyo janga la virusi vya corona limempa mamlaka mahsusi. Sasa sheria ya hali ya hatari inatumika.

Uchaguzi huru wa kwanza uliokuwa ufanyike mnamo mwaka huu umeahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na janga la corona. Hata hivyo jimbo la Tigray limesema halifuati amri hiyo na kwamba uchaguzi utafanyika mnamo mwaka huu. Majimbo mengine kama vile la Oromo linaweza kufuata mkumbo.

Watuhumiwa watatu wamekamatwa na wako mahabusu

Waziri Mkuu Abiy Ahmed amesema mwanamuziki Hachalu ameuawa na watu wanaopinga mageuzi kutoka ndani na nje ya Ethiopia. Watuhumiwa watatu wamekamatwa na wako mahabusu, ikiwa pamoja na wapinzani mashuhuri Jawar Mohammed na Bekele Gerba. Mageuzi ambayo Waziri Mkuu Abiy Ahmed ameyaanzisha yameleta matumaini ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Dr. Abiy Ahmed
Waziri Mkuu Abiy AhmedPicha: DW/S. Teshome

Pana hofu ya kumwagika damu zaidi nchini Ethiopia. Abiy anapaswa kutafuta njia ya kuleta maridhino ya kitaifa kwa njia ya mdahalo na watu wa kabila la Oromo wanapaswa kuitikia mwito wa maridhiano. Pande zote zinapaswa kutafuta suluhisho la kitaifa kuvuka siasa za kifalme, itikadi za dini na za kikomunisti hata Nelson Mandela alijua kwamba hakuna taifa linaloweza kuundwa katika msingi wa visasi.