Mnamo mwaka 2011 rais wa Syria Bashar al Assad na serikali yake ilionekana kama utawala uliokaribia kuanguka kufuatia wimbi la mapinduzi ya kupigania demokrasia yaliyoshuhudiwa katika nchi za eneo la Mashariki ya Kati. Miaka kumi baadaye Assad bado yupo madarakani, huku amani ya Syria ikiwa bado kitendawili. Karibu tujadili hayo na mengine mengi kwenye kipindi cha Maoni. Nahodha ni Josephat Charo.