Maoni: Syria na makosa ya mataifa ya magharibi
15 Machi 2018Uhakika lakini ni kwamba , Mataifa ya magharibi yamepata funzo kutokana na makosa yake.
Vita vya Syria ni suala linalohitajika kujadiliwa na wataalamu wa historia katika mtaala maalum wa historia ya mambo ya kubuni: Kitu gani kingetokea iwapo..... ? Hususan swali hili linaweza kuulizwa kwa kuyatazama mataifa ya magharibi: Vita hivi vingeendaje , iwapo vingeshughulikiwa vinginevyo tofauti na vilivyoshughulikiwa? Swali hilo bila shaka halina jibu.Linawahusu watu kadhaa ambao wameathirika , ambao iwapo mataifa ya magharibi yangelishughulikia vita hivi tofauti na walivyofanya, huenda , wangekuwa bado wanaishi.
Kwa mtazamo wa sasa hivi historia ya maamuzi hususan ya mataifa ya magharibi ni nafasi iliyopotea. Baadhi wamekiri katika mwaka 2013, walipotambua kuwa utawala wa rais Bashar al-Assad huenda ulitumia gesi ya sumu dhidi ya wananchi wake, na rais wa Marekani Barack Obama akatahadharisha juu ya kile alichokiita "mstari mwekundu", ambao katika hatua hii ulikwisha vukwa na kuonya kwamba atachukua hatua. Alipuuzia kuhusu sumu ama onyo lake, ama yote mawili.
Kwa hiyo , inaonesha , kulikuwa na uwezekano wa fursa ya mwisho , kuuonesha utawala wa Assad mpaka wake. Wakati huo kulikuwa hakuna nchi zilizokuwa zinautetea utawala huo kama Iran na Urusi, na sio katika hali ambayo nchi hiyo inajikuta hivi sasa. Kwa hivi sasa katika kila eneo kuna uwiano wa nguvu kubwa kabisa, kama ilivyo kwa Marekani na washirika wake. Obama alipoteza uwezekano huo.
Sababu sahihi kabisa
Wakati huo alikuwa na sababu nzuri tu. Kuingilia kati kwa Marekani nchini Iraq kulitokea miaka 10 tu iliyopita, na kwa muda mferu ilikuwa ni maafa kisiasa, kimaadili na kipropaganda.
Wendawazimu, kwa misingi ya uongo mkubwa walifanya uvamizi na kuiweka Marekani kuwa utawala wenye kiburi, mabeberu mamboleo , hali inayoonesha kwamba hadi leo hawajaweza kujitoa.
Ndio sababu miaka kumi baadaye , uvamizi mwingine katika mashariki ya kati , mara hii Syria, ni jambo la hatari.
Kama ingetokea hadhi ya Marekani ingeharibika zaidi. Pamoja na kwamba hali hiyo ilikuwa ngumu lakini hatari ya kimkakati , ilikuwa si sahihi, kuliko hatua ya kuingilia kati ingefanyika. Assad angeacha athari yoyote ? Iran na Urusi zingethubutu kupambana na uvamizi huo ? Na Obama angeweza kuvutia sehemu ya mataifa ya Kiislamu , Washia pengine lakini hata Wasuni ?
Uvamizi mwingine ungekuwa na maana ya mashambulio mapya ya wapiganaji wa jihadi nchini Marekani ama hata barani Ulaya? Inawezekana kabisa kwamba uvamizi mwingine ukaleta matokeo mabaya zaidi. Hali ya sasa inafahamika lakini Urusi na Iran zimekamata udhibiti na kuingilia kati , hadi mapambano na mataifa ya magharibi hayawezekani tena.
Mwandishi: Knipp, Kersten /ZR/ Sekione Kitojo
Mhariri: Daniel Gakuba