Maoni: von der Leyen ndie rais mpya wa halmashauri ya Ulaya
17 Julai 2019Mhariri anaandika kuwa mara hii ilikuwa tofauti, ilikuwa siku ambapo mgombea huyo kutoka Ujerumani kila kitu kiliwezekana. Alilazimika kulidhibiti jukwaa la bunge la Ulaya. Akalazimika kuwashawishi wale waliokuwa wakimtilia shaka, akaliimarisha kundi la wale waliokuwa wakimuunga mkono, na wapinzani akawaweka katika njia ambamo wanaweza kumuunga mkono. Na anatakiwa kushughulikia masuala ya Ulaya.
Kila kundi lilimpigia kura Ursula von der Leyen, hata kama hatimaye ulikuwa ushindi mwembamba kwa kura tisa tu. Mwanamke huyu mwenye msimamo wa utetezi wa wanawake alijionesha kuwa ni mtetezi wa masuala ya kijamii na mlinzi wa mazingira kama wengi wa wanachama wenzake katika chama chake, na alionesha kujiamini na kwamba ni mwanamke anayeweza.
Huenda lilikuwa wazo lake bora hotuba yake kuizungumza katika lugha tatu. Kifaransa kutokana na hisia za nguvu za uwakilishi wa umma, Kiingereza, kutokana na ukweli ulio mgumu pamoja na mahitaji, kutokana na kiwango kikubwa cha uendeshaji wa uchumi mkubwa na kupata haki sawa wa kijinsia.
Wajerumani walimchagua baada ya kufikia uamuzi kuwa mwanasiasa huyo aliyezaliwa mjini Brussels, majaaliwa yake ni kama yameelekezwa katika kufanyakazi katika Umoja huo.
Si siri tena, kwamba von der Leyen kwa wadhifa huu alikuwa ni chaguo la pili. Anafahamu , kwamba anapaswa kupambana na hali hii. Angeweza kupoteza kila kitu. Lakini ameleta mshangao na kutoka kuwa chini amejiweka juu. Amewaacha hoi wale ambao hawapendelei Umoja wa Ulaya na wale wanaotaka kujitoa kutoka Umoja huo. Njia hii ni lazima aiendeleze na kulizuwia kundi la mrengo wa kulia.
Hayo yote , hata hivyo hayahakikishi kuwa na urais wa mafanikio katika halmashauri ya Umoja wa Ulaya , lakini ni mwanzo mzuri na ni siku nzuri kwa bunge la Ulaya, kwamba kulikuwa na uchaguzi halisi.
Kundi ambalo limeshindwa kwa kiasi kikubwa katika siku hii ya uchaguzi ni wabunge wa Ulaya wa Ujerumani wa kutoka wa chama cha Social democratic. Walitaka kwa njia zote kuwe na makubaliano ya mgombea wao ashike wadhifa huo.