1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano dhidi ya kundi la IS yapamba moto Syria

Admin.WagnerD13 Februari 2019

Wanamgambo wa itikadi kali wanaojiita "Dola la kiislam"-IS wanajaribu kuiokoa ngome yao ya mwisho mashariki mwa Syria leo jumatano huku wake na watoto wao wakiyapa kisogo mapigano makali katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/3DJZO
Syrien IS - Kampf um Baghus -  Rauchwolken über der Provinz Deir Al Zor
Picha: Reuters/ANHA

Vikosi vya  wanamgambo wa kiarabu na kikurdi vinavyopigania kidemokrasi nchini Syria, SDF vimeanzisha opereshini kubwa jumamosi iliyopita kwa lengo la kuwatimua wapiganaji wa  dola la kiislam , IS au Daesh kutoka ngome yao ya mwisho miongoni mwa ngome walizokuwa wakizizidhibiti tangu mwaka 2014 nchini Syria na Iraq.

Maelfu ya watu wamekuwa wakikimbia mnamo siku za hivi karibuni kutoka kile kinachojulikana kama eneo la Baghouz", karibu na mpaka wa Iraq, wengi wao ni wanawake na watoto, ingawa wanamgambo  wa itikadi kali pia ni miongoni mwao.

Tangu decemba mwaka jana zaidi ya watu 38.000, wengi wao wake na watoto wa wapiganaji wa itikadi kali wameyapa kisogo maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na IS.

"Tumevikomboa vituo kadhaa vilivyokuwa hapo awali vikidhibitiwa na IS". msemaji wa vikosi vinavyopigania demokrasi nchini Syria, SDF, Mustafa Bali amesema.

Vikosi vya Kikurdi vinasonga mbele taratibu

Irak - arabische Einheit der SDF und türksiche Truppen gegen den IS
Picha: picture-alliance/NurPhoto/S. Backhaus

Shirika la Syria linalosimamia masuala ya haki za binaadam limesema wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani wanasonga mbele kidogo kidogo. "Miripuko imetegwa kila mahala katika eneo hilo" amesema kiongozi wa shirika hilo lenye makao yake nchini Uingereza, Rami Abdul Rahman.

Vikosi vya SDF vinafyetua mizinga amesema na kuongeza " mapigano makali yamepamba moto katika kila pembe ya kijiji cha Baghouz.

Vikosi vinavyopigania demokrasia nchini Syria SDF vimeanzisha opereshini ya kijeshi kuwatimua wapiganaji wa itikadi kali wa Is toka mkoa tajiri kwa mafuta wa Deir Ezzor tangu septemba mwaka jana.

Tangu wakati huo zaidi ya wapiganaji 1300 wa SDF na wanajihadi 650 wameuliwa huku raia zaidi ya 400 wakipoteza pia maisha yao.

Kutakuwa na ushindi hivi karibuni?

Rais Donald Trump wa Marekani aliashiria uwezekano kwa vikosi vya muungano kutangaza ushindi mnamo siku chache zinazokuja dhidi ya IS.

USA Präsident Donald Trump
Picha: Reuters/J. Young

Ushindi wa vikosi hivyo katika kijiji cha Baghouz utaiwezesha Marekani kuwahamisha wanajeshi wake 2000 kutoka Syria, kama alivyotangaza rais Trump decemba mwaka jana.

"Tunaambatana na wakati ili kuweza kuheshimu ahadi tuliyotoa" amesema kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan alipokuwa ziarani nchini Iraq jana bila ya kutaja lini hasa wanajeshi wa Marekani wataondolewa Syria.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri: Iddi Ssessanga