1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaingia siku ya nne nchini Nigeria

29 Julai 2009

Mapigano kati ya Wanamgambo wa Kiislamu na Vikosi vya Usalama vya Nigeria leo yaingia siku ya nne.

https://p.dw.com/p/IzTl
Baadhi ya Waliyokamatwa wakiwa katika kituo cha polisi huku pembeni kukiwa na maiti za waliouwawa kutoka na mapigano yanayoendelea.Picha: AP

Mapigano makali kati ya Vikosi vya Usalama na Kundi la Waislamu wenye msimamo mkali leo hii yameingia siku ya nne huko Kaskazini mwa Nigeria ambapo vikosi hivyo hivyo sasa vimekuwa katika msako mkali wa kuwatafuta wapiganaji wa kundi hilo.

Takwimu zisizo rasmi mpaka sasa zinaonesha kuwa zaidi ya watu 250 wamepoteza maisha kufuatia mapigano hayo yaliyoanzia katika mji wa Bauchi uliyopo Kaskazini mwa Nigeria.

Sauti za milio ya risasi zimesikika usiku kucha katika jimbo la Maiduguri eneo ambalo limekuwa kama kambi ya Wapiganaji hao wanaofuata mtindo wa Wanamgambo wa Talibani.

Kutokana na amri ya Rais wa Umar Yar'Adua Vikosi vya ulinzi vimeonekana mitaani mara kadhaa vikikabiliana na Wanamgabo hao.

Tangu kutolewa kwa kauli hiyo pamoja na wananchi kuziwa kutoka nje lakini hali imeendelea kuwa mbaya.

Mapema jana, nyumbani kwa kiongozi wa Kidini wa Kundi hilo Mohammed Yusuf ambapo kulionekana idadi kubwa ya Wafuasi wa kundi hilo kulizingirwa na polisi lakini hakuna taarifa madhubuti za kiongozi huyo kukumbwa na dhahama yeyote.

Mkazi mmoja wa Maiduguri Abdul Mimini Hassan amesema mapigano makali yalishika kasi usiku kucha na kwamba eneo ambalo vikosi vya serikali vilikuwa vikielekeza mashambulizi ni katika Bayan Quartes eneo ambalo linapakana na nyumba ya Yusuf.

Mkazi huyo amesema baada ya milio ya risasi kutulia katika eneo hilo muda mfupi baade ikaanza kuvuma kutoka upande mwingine wa karibu na hapo uliyo wa mkabala huo wa Ungwani.

Maiduguri ambao ni mji mkuu wa Jimbo la Borno limekuwa jimbo lisilokalika kwa kuwa na mapigano makali tangu kuibuka kwa machafuko hayo jumapili iliyopita katika jimbo la Bauchi.

Mapambano ya kwanza yalizuka baada ya Polisi kumjeruhi Mwanamgambo wa Waislamu hao wenye msimamo mkali na baadae yakaenea kwa kasi katika majimbo mengine manee yaliyo Kaskazini mwa Nigeria.

Serikali tayari imetnagaza idadi ya waliyokufa katika majimbo ya Bauchi na Yobe kuwa ni 55 lakini idadi kubwa ya maafa yametokea katika mji wa Maiduguri eneo ambalo kwa takwimu za Jeshi la Polisi za jumatatu watu 206 wamekufa.

Taarifa ya vyombo mbalimbali vya habari zinaonesha kuwa wengi waliyokufa ni Vijana wenye umri usiyozidi miaka 20 waliyokatika kundi la Waislamu wenye msimamo mkali.

Mapaigano kama hayo yalitokea Novemba mwaka uliyopita kati ya Waislam na Wakristo ambapo wanaharakati wa haki za binadamu walisema zaidi ya watu 700 waliuwawa.

Tangu kurejea kwa utawala wa kiraia nchini Nigeria mwaka 1999 majimbo 12 yaliyo Kaskazini mwa nchi hiyo yamekuwa yakitumia sheria za kiislamu jambo ambalo limekuwa likizusha migogoro ya mara kwa mara.

Mwandishi-Sudi Mnette AFPE

Mhariri.M. Abdul-Rahman.