1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yamezuka kati ya Armenia na Azerbaijan

28 Septemba 2020

Majeshi ya Armenia na Azerbaijan  yameingia katika siku ya pili ya mapigano makali ya kutumia nguvu za kijeshi, huku kukiwa na ripoti ya vifo na idadi kubwa ya waliojeruhiwa.

https://p.dw.com/p/3j6IY
Aserbaidschan I Zerstörtes Haus in Tartar
Picha: Ibrahim Hashimov/Sputnik/dpa/picture-alliance

Mirindimo ya makombora kutoka angani ilizizima jana, katika eneo la mji mkuu wa Step-ay-nakert, kufuatia mzozo huo wa  Nagorno-Karabakh ambao unaonekana  sasa kuwa kama vita kamili. Kila upande sasa unautupia lawama mwingine kufuatia matumizi ya makombora, huku kukigubikwa na taarifa ya kwamba takribani watu 21 wameuawa na wengine mamia kujeruhiwa. Mzozo huo unatokana na kufuatia mzozo wa jimbo lililojitenga la Nagorno-Karabakh.

Wasiwasi mpya ya amani katika eneo la kusini mwa Caucasus.

Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan, ambayo yanaonekana makubwa kabisa kutokea tanmgu 2016, yanazusha wasiwasi katika ukanda wa Kusini mwa Caucasus, eneo ambalo kumepitisha bomba kubwa la mafuta na gesi kuelekea katika maeneo ya soko la ulimwengu. Mataifa hayo mawili ya zamani ambayo yalikuwa katika uliokuwa Umoja wa Kisovieti, yamekuwa yakikabiliana katika vipindi tofauti kwa takribani muongo mmoja. Mzizi wa yote ulikuwa jimbo la Nagorno-Karabakh. Eneo hilo kimsingi lipo ndani ya Azerbaijan lakini likiendeshwa na jamii ndogo ya Waarmenia.

Armenien Yerevan | Militär rekrutiert Freiwillige
Wanajeshi wa Armenia mkutanoniPicha: Melik Baghdasaryan/Reuters

Rais wa Azerbaijan ametangaza kuanza kwa operesheni za kiasi za kijeshi huku waziri wake wa mambo ya ndani akisema raia sita wa taifa hilo wameuwawa na wengine 19 wamejeruhiwa tangu kuzuka kwa mapigano hayo. Shirika la habari la Interfax limemnukuu mwakilishi wa wizara ya ulinzi akisema Waarmenia 200 wamejeruhiwa. Lakini katika eneo la Nagorno-Karabakh kumeripotiwa zaidi ya wanajeshi 15 kuuwawa pamoja na kupotezwa kwa udhibiti wa jimbo hilo na hasa kutokana na ongezeko la mashambilizi ya Azerbaijan.

Soma zaidi:Mapambano yazuka kati ya majeshi ya Armenia na Azerbaijan

Wakati hayo yakiendelea, bunge la Armenia muda mfupi uliopita limeitupia lawama Uturuki kwa kusababisha machafuko katika ukanda huo. Awali pia balozi wa Armenia nchini Urusi alisema Uturuki imepeleka wapiganaji 4,000 kutoka eneo la kaskazini mwa Syria, ambao wanashiriki katika mapigano, habari ambayo hata hivyo ilikanushwa na ofisi wa rais wa Azerbaijan.

Vyanzo: RTR