1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Maporomoko ya ardhi kaskazini mwa Pakistan yafukia malori 20

18 Aprili 2023

Malori yapatayo 20 yamefukiwa kwenye mporomoko ya ardhi kaskazini magharibi mwa Pakistan. Hali hiyo ilitokea baada ya barabara kuu inayopitia katika eneo la Khyber kukumbwa na mvua kubwa zilizosababisha dhoruba kali

https://p.dw.com/p/4QEHq
Pakistan | Erdrutsch auf einer Autobahn nahe der Grenzstadt Torkham
Picha: Muhammad Sajjad/AP Photo/picture alliance

Malori yapatayo 20 yamefukiwa kwenye mporomoko ya ardhi kaskazini magharibi mwa Pakistan. Hali hiyo ilitokea baada ya barabara kuu inayopitia katika eneo la Khyber kukumbwa na mvua kubwa na radi  zilizosababisha dhoruba kali. 

Naibu kamishna wa wilaya hiyo ya Khyber Abdul Nasir Khan ameliambia shirika la Habari la Reuters kwamba raia wawili wa Afghanistan wamekufa na watu wengine watatu wamepelekwa hospitalini huku wakitarajia idadi ya watu waliojeruhiwa kuongezeka. Amesema kazi ya uokoaji inaendelea.

Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea alfajiri ya leo Jumanne katika njia kuu inayounganisha Pakistan na Afghanistan.