1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Maporomoko ya ardhi yauwa, yajeruhi Ufilipino

7 Februari 2024

Maporomoko ya ardhi yamewauwa watu sita na kuwajeruhi wengine 31 katika mkoa wa kusini mwa Ufilipino usiku wa kuamkia Jumatano (Februari 7).

https://p.dw.com/p/4c7dJ
Rais Ferdinand Marcos Jr. wa Ufilipino.
Rais Ferdinand Marcos Jr. wa Ufilipino.Picha: Eloisa Lopez/REUTERS

Kulingana na maafisa wa kukabiliana na majanga nchini humo, nyumba kadhaa zimezikwa pamoja na mabasi mawili yaliyokuwa yamewabeba abiria 27.

Maporomoko hayo yalitokea katika mkoa wa Davao de Oro wenye mgodi wa dhahabu, ambapo mabasi yalikuwa yanawabeba wafanyakazi wa mgodi huo.

Soma zaidi: Kimbunga Hagupit chaleta madhara Ufilipino

Jumla ya watu 46 hawajulikani walipo.

Katika taarifa yake, shirika la kukabiliana na majanga lilisema zaidi ya familia 700 katika maeneo yaliyoathirika zimeokolewa.

Takwimu za shirika hilo pia zinaonesha kuwa upepo wa msimu kutoka Bahari ya Hindi uliopiga kutoka kaskazini mashariki ulisababisha mvua kubwa na mafuriko kati ya Januari 28 na Februari 2.