1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPapua New Guinea

Papua New Guinea haina makubaliano ya usalama na China

11 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea amesema hakujawahi kufanyika mazungumzo ya masuala ya ulinzi na China, baada ya taifa hilo lenye utajiri wa rasilimali kusaini makubaliano ya usalama na jirani yake, Australia.

https://p.dw.com/p/4a040
Waziri Mkuu wa Papua New Guinea, James Marape.
Waziri Mkuu wa Papua New Guinea, James Marape.Picha: Lukas Coch/AAP/dpa/picture alliance

James Marape alisema siku ya Jumapili (Disemba 10) kwamba nchi yake imekuwa ikifanya mambo yake kwa uwazi, na kwamba alipoitembelea Beijing mwaka huu akiwa na mawaziri yake, hakikuwa na mazungumzo yoyote kuhusiana na mambo ya ulinzi na usalama.

Kwenye mkutano wake na wawekezaji mjini Sydney, kiongozi huyo wa New Papua Guinea alisema uhusiano wao na China ni masuala ya kiuchumi. Mnamo mwezi Mei, nchi hiyo ilisaini makubaliano ya ulinzi wa nje na Marekani, na wiki iliyopita ikafikia makubaliano ya usalama wa ndani na Australia.