Marekani kuongeza misaada kwa waathiriwa wa tetemeko Japan
5 Januari 2024Wajima,
Marekani imesema kuwa inajiandaa kupeleka misaada zaidi katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi nchini Japan lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 90 na kulazimisha watu wengine 33,000 kukimbia makaazi yao.
Balozi wa Marekani nchini Japan Rahm Emmanuel ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kuwa, Washington iko tayari kumsaidia rafiki na mshirika wake wa karibu kufuatia tetemeko la ardhi.
Msemaji wa serikali ya Japan Yoshimasa Hayashi amesema nchi hiyo kwa wakati huu imekataa misaada kutoka mataifa kadhaa iliyojitolea kuisaidia ikiwemo China.
Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Ritcha liliipiga eneo la Noto nchini Japan siku ya mwaka mpya na kuharibu nyumba, miundo mbinu na kusababisha ugumu wa kusafirisha misaada ya kibinadamu katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo.