1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Iraq kujadiliana kuhusu vikosi vya jeshi

26 Julai 2021

Rais wa Marekani Joe Biden, atakuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhemi leo ambapo anatarajiwa kuzindua kile kinachoitwa "awamu mpya" ya uwepo wa jeshi la Marekani nchini Iraq.

https://p.dw.com/p/3y5An
Irak Ausbildung Soldaten durch US Militär
Picha: picture-alliance/dpa/K. Al-A'nei

Kimsingi hatua hii inafikisha mwisho shughuli za kijeshi lakini sio kujiondoa kabisa kwa majeshi ya Marekani nchini humo. 

Uwepo wa vikosi vya Marekani nchini Iraq utakuwa kiini cha mkutano kati ya rais Biden na Kadhemi, kiongozi ambaye yuko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa vikundi vyenye silaha vya Tehran ambavyo vinataka kuondolewa kwa wanajeshi 2,500 wa Marekani ambao bado wapo Iraq. soma Idadi ya waliokufa nchini Iraq kwenye shambulizi yafikia 32

Lakini swali ni ikiwa Baghdad inaweza kukabiliana na kundi lenye itikadi kali linaloojiita Dola la kiislamu IS.

Wiki iliyopita IS ilidai kuhusika na shambulio la kujitoa muhanga katika soko la Baghdad ambalo liliwaua watu 30, licha ya maafisa wa Iraq kutangaza kuwa Wasunni wenye msimamo mkali walisambaratishwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Iraq bado inahitaji mafunzo endelevu

Irak Bagdad | Anschlag | Al-Wahilat Markt
Picha: Murtadha Al-Sudani/Anadolu Agency/picture alliance

Afisa mwandamizi wa utawala wa Biden amesema Iraq imeomba, na wamekubali, kwamba wanahitaji mafunzo endelevu, msaada na vifaa, ujasusi, kujenga uwezo wa ushauri, na yote haya yataendelea.

Wanajeshi wengine 2,500 wa Marekani bado wamebaki Iraq kama sehemu ya muungano wa kupambana na IS, na mbali na hao kuna vikosi maalum vya ziada, ambavyo idadi yao haijulikani. Soma Marekani yashambulia maeneo ya wapiganaji Syria

Huku ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa bunge, Kadhemi ambaye nchi yake imeharibiwa na vurugu, umasikini na ufisadi, anatarajia kupata nguvu akiwa na vikundi vidogo vyenye nguvu vinavyounga mkono Iran, ambavyo vina uhasama mkubwa kwa uwepo wa Marekani.

Mashambulizi ya mara kwa mara

Deutschland AP Kriegsfotografin Anja Niedringhaus Foto Irak
Picha: picture-alliance/AP

Vikosi vya Marekani vilivyoko Iraq vimekuwa vikiendelea kushambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wanaounga mkono Iran, ambao nao wamelipizwa kwa mashambulizi na jeshi la Marekani.  Jeshi la Marekani lawashambulia wanamgambo Iraq na Syria

Iraq ni kiungo muhimu cha kimkakati kwa Marekani, ambayo inaongoza umoja wa kimataifa unaopambana na kundi la IS katika nchi jirani ya Syria. Na kuiacha Iraq kwenye ushawishi wa Iran sio jambo sahihi kwa Marekani. Washington na Tehran zimejaa mivutano mipya hata ikiwa Biden ameashiria utayari wake wa kurudi kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran ya 2015.

Ramzy Mardini, mtaalamu wa siasa za Iraq katika Chuo Kikuu cha Pearson huko Chicago, anaamini mkutano wa Biden na Kadhemi unaweza kujengwa ili kumsaidia Waziri Mkuu wa Iraq kupunguza shinikizo za nyumbani, lakini mambo yatakavyokuwa nyanjani yataonyesha hali ilivyo na uwepo wa kudumu wa Marekani.

 

Vyanzo//AFPE, APF