Marekani na Kenya zasaini makubaliano ya ulinzi
26 Septemba 2023Chini ya makubaliano hayo, Kenya itaongoza ujumbe wa kimataifa wa kulinda amani nchini Haiti utakaokuwa na jukumu la kupambana na magenge yanayosababisha machafuko nchini humo.
Makubaliano hayo ya ulinzi kati ya Marekani na Kenya yalisainiwa jana Jumatatu kati ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, na mwenzake wa Kenya, Aden Duale, katika mkutano uliofanyika jijini Nairobi.
Soma pia:Marekani imeahidi kutoa dola milioni 100 kwa Haiti
Austin amesema serikali ya nchi yake itashirikiana na bunge kupata dola millioni 100 kwa ajli ya shughuli za kijeshi za kulinda amani nchini Haiti.
Makubaliano hayo ya Marekani na Kenya yatatowa mwelekeo wa sera ya ulinzi katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili kwa kipindi cha miaka mitano, wakati vita dhidi yakundi la al-Shabaab linalofungamanishwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida katika eneo la Afrika Mashariki vikiongezeka.