Marekani na Korea Kusini zaboresha makubaliano ya kijeshi
13 Novemba 2023Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin yuko mjini Seoul kushiriki mkutano wa mwaka wa usalama pamoja na mwenzake wa Korea Kusini Shin Won-sik, wakati washirika hao wakiimarisha ushirikiano wa kiulinzi katikati ya ongezeko la vitisho vya makombora na nyuklia kutoka Pyongyang.
"Tumejaribiwa kila wakati, na tumedhibiti kila changamoto. Kwa pamoja, tulijenga mojawapo ya ushirikiano imara zaidi na wenye uwezo mkubwa ulimwenguni. Tumezuia migogoro na uchokozi mkubwa kwenye Rasi ya Korea kwa miongo saba. Ni muhimu, na tutaendelea kuwa tayari kupambana," alisema Austin.
Kulingana na taarifa, mabadiliko kwenye makubaliano hayo yaliyofikiwa mwaka 2013 yanamaanisha, kuanzia sasa yataruhusu washirika hao kuzuia kwa ufanisi zaidi hatua za Korea Kaskazini za kuendeleza mipango yake ya nyuklia na isiyo ya nyuklia yenye athari za kimkakati.