MigogoroNiger
Niger yajadiliana na Marekani juu ya kuondoa wanajeshi wake
25 Aprili 2024Matangazo
Utawala wa kijeshi wa Niger umeiomba Marekani kuwaondoa wanajeshi wake waliomo nchini humo kutokana na kutoelewana kuhusu masuala kadhaa ambayo ni pamoja na kushindwa kutambua hatua zilizopigwa na taifa hilo kuelekea utawala wa kidemokrasia.
Hadi mapinduzi ya mwaka jana Niger ilikuwa mshirika mkubwa wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi na wanajeshi hao wamekuwa wakitoa mafunzo kwa vikosi vya nchini humo kupambana na makundi ya wanamgambo.
Chanzo chenye uelewa na suala hilo wiki iliyopita kilisema Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Kurt Campbell na utawala wa Niger wamekubaliana juu ya hatua hiyo.