Marekani yaanza tena kutoa msaada wa chakula Ethiopia
15 Novemba 2023Tangazo hilo limejiri ikiwa ni miezi mitano baada ya kusitisha mpango wake wa kitaifa kutokana na ufisadi mkubwa uliofanywa na maafisa wa nchini Ethiopia.
Msemaji wa USAID Jessica Jennings amesema kurejeshwa kwa shughuli hizo za misaada kumetokana na mageuzi mapya yaliyofanywa na shirika hilo ili kuimarisha usajili wa wanufaika na ufuatiliaji wa nafaka zinazotolewa.
Jeshi la Ethiopia larejesha udhibiti mji wa Lalibela
Amesema hatua hizo mpya zitajaribiwa kwa mwaka mmoja, akiongeza kuwa zitabadilisha pakubwa mfumo wa msaada wa chakula nchini Ethiopia na kusaidia kuhakikisha kuwa msaada unawafikia wanaokumbwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Mwezi uliopita USAID ilianza tena kutoa msaada wa chakula kwa wakimbizi milioni moja baada ya serikali ya Ethiopia kukubali kujiondoa katika shughuli za utolewaji, uhifadhi na usambazaji wa msaada wa chakula cha wakimbizi.