Marekani yabaini idadi ndogo ya Wayazidi Iraq
14 Agosti 2014Marekani imekuwa ikitafakari ikitoa uzito katika masuala kadhaa ikiwemo kuwadodoshea vyakula, watu wa jamii ya wachache ya Wayazidi ambao walikimbia makazi yao baada ya maeneo yao kudhibitiwa na kundi linalojiita Dola ya Kiislamu.
Kwa takribani siku nne, maelefu ya watu kadhaa walihofiwa kuwepo katika eneo la mlima pasipo malazi na kiasi kidogo cha chakula na maji. Marekani ilifanya mashambulizi ya anga kuvuruga nguvu za wanamgambon hao, huku Wamerkani hao kwa kushirikiana na Uingereza na jeshi la Iraq walifanya kazi ya kuwadodoshea mahitaji muhumu wakimbizi.
Kilichobainiwa na wachunguzi
Msemaji wa Wizara wa jeshi la Marekani, John Kirby alisema tumu ya watu wasiozidi 20,raia watoa misaada, maafisa wa jeshi wametumia siku nzima katika eneo la mlima Sinjar kwa ajili ya kutathimini namna hali ilivyo. Kirby amesema idadi ya watu iliyokutwa katika eneo hilo ilikuwa ndogo kulikuo ilivyodhania awali.
Aidha alisifu zoezi la utoaji misaada ya kiutu na kuongeza kuwa idadi hiyo ya watu iliweza kutoroka katika eneo hilo katika kipindi cha giza na kwamba idadi hiyo ndogo ya watu waliosalia katika eneo hilo wanaendelea vyema na wanapata mahitaji kuliko ilivyofikiria awali. Marekani pia imesisitiza kuendelea kutoa misaada ya kiutu.
Mkutano wa dharura wa Umoja wa Ulaya
Katika hatua nyingine mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya kesho watafanya mkutano wa dharura wenye lengo la kujadili kwa masharti gani wataweza kuwasilisha silaha kwa mamlaka ya Kikurd ili waweze kukabiliana na wanamgambo wa Dola la Kiislamu.
Na Umoja wa Mataifa hapo jana umelaani vikali vitendo vya ubakaji vinavyodaiwa kufanywa na wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Mwakilishi Maamulu waumoja huo nchini Iraq Nikolay Mladenov amaeitolewa mwito jumuiya ya kimataifa kusaidia serikali ya Iraq katika kuwanusuru wanawake na watoto wanaoshikiliwa mateka.
Mapigano bado yanaendelea huko magharibi mwa Baghad ambapo maafisa wa afya wanasema watoto wanne wameuwawa katika mapigano kati ya wanamgambo wa madhehebu ya Sunni na wanajeshi wa Iraq. Mkurugenzi wa hospitali Ahmed Shami alisema mapigano hayo yalitokea mapema leo katika viunga vya mji wa kaskazini wa Fallujah, ambao umekuwa mikononi mwa wapiganaji wa Dola la Kiislamu tangu Januari.
Shami alisema kiasi ya wanamgambao 10 na wanawake vilevile wameuwawa. Hakuna na maelezo zaidi kuhusu makasa huo lakini alisema miili ya marehemu hao iliwasilishwa hospitali. Pamoja na Falluja, mji ambao upo kilometa 65 magharibi mwa Baghad, Dola la Kiislamu lindhibiti eneo kubwa la kaskazini na mashariki.
Mashumbulizi ya wanamgambo yameiingiza Iraq katika machafuko makubwa kabisa kuwahi kutokea tangu kuondoka kwa majeshi ya marekani katika ardhi ya taifa hilo.
Mwandishi: Sudi Mnette APE/DPA
Mhariri: Iddi Ssessanga