US yachunguza kuvuja nyaraka za shambulio la dhidi ya Iran
20 Oktoba 2024Akizungumza na shirika la habari la CNN la Johnson ameeleza kuwa wanalifuatilia kwa karibu suala hilo bila ya kutoa taarifa zaidi. Kulingana na afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutajwa jina, nyaraka zilizovuja zinaonekana kuwa halali.
Soma zaidi: Israel yasema 'maslahi ya taifa' kwanza katika kuijibu Iran
Nyaraka hizo zilizokuwa na mhuri unaoonesha kuwa ni za siri, zilichapishwa kwenye jukwaa la Telegram na kisha ziliripotiwa pia na vituo vya Habari vya CNN na Axios.
Soma zaidi:Iran yaahidi kuishambulia miundo mbinu ya Israel iwapo itashambuliwa
Upelelezi una unaofanywa kuhusu kuvuja kwa taarifa hizo unachunguza pia namna nyaraka hizo zilivyopatikana aidha kwa makusudi, au kwa njia nyingine kama vile udukuzi. Kama sehemu ya uchunguzi huo, maafisa wanachunguza pia kufahamu mtu aliyehusika kuzipata nyaraka hizo kabla ya kuchapishwa.