1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yapanga kuiuzia Israel silaha za dola bilioni 8

4 Januari 2025

Utawala wa rais Joe Biden umeliarifu kwa njia isiyo rasmi Bunge la Marekani kuhusu mpango wa uuzaji wa silaha kwa Israel wenye thamani ya dola bilioni 8 unaojumuisha silaha za ndege za kivita.

https://p.dw.com/p/4ooUW
Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya F-15
Mpango huo wa Marekani unajumuisha silaha zinazotumiwa kwenye ndege za kivita na helikopta za mashambulizi.Picha: Alexander Vasquez/U.S Air/picture alliance

Utawala wa rais Joe Biden umeliarifu kwa njia isiyo rasmi Bunge la Marekani kuhusu mpango wa uuzaji wa silaha kwa Israel wenye thamani ya dola bilioni 8 unaojumuisha silaha zinazotumiwa kwenye ndege za kivita na helikopta za mashambulizi.

Hata hivyo, mkataba huo utahitaji idhini kutoka kwa Baraza la Bunge na Seneti na unajumuisha makombora ya anga yanayotumiwa kujilinda dhidi ya vitisho kama vile mashambulizi ya droni. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani haijazungumzia lolote kuhusu mpango huo.

Hayo yanajiri wakati Israel ikiendelea kupambana na kundi la Hamas pamoja na waasi wa Kihouthi wa Yemen ambao wamekuwa wakifanya mara kadhaa mashambulizi ya makombora na droni kuelekea Israel. Juhudi za kidiplomasia hadi sasa zimeshindwa kukomesha vita vya miezi 15 katika Ukanda wa Gaza.