1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Marekani yasikitishwa na ombi la Mali kuhusu tume ya MINUSMA

20 Juni 2023

Marekani imeelezea masikitiko yake kuhusu uamuzi wa utawala wa mpito wa kijeshi wa Mali kukitaka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kiondoke nchini humo.

https://p.dw.com/p/4SoQv
Symbolbild I MINUSMA in Mali
Picha: Sia Kambou/AFP

Marekani imeelezea masikitiko yake kuhusu uamuzi wa utawala wa mpito wa kijeshi wa Mali kukitaka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kiondoke nchini humo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na wizara ya mambo ya nje ya Marekani ikitaka pawepo na utaratibu na uangalifu katika mchakato mzima wa kuwaondoa wanajeshi wa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA.

Waziri wa mambo ya nje wa Mali Abdoulaye Diop aliwasilisha ombi hilo katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa akitaja kuwepo na mgogoro kutokana na kukosekana uaminifu kati ya mamlaka za Mali na tume ya MINUSMA.