SiasaGabon
Marekani yasimamisha msaada kwa Gabon kufuatia mapinduzi
24 Oktoba 2023Matangazo
Marekani imesema imesitisha msaada kwa Gabon kufuatia mapinduzi yaliyofanyika Agosti 30 nchini humo.
Kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Mathew Miller, Marekani ambayo ilikuwa tayari imesitisha misaada kwa nchi hiyo, kwa sasa imebaini rasmi kwamba mapinduzi yalifanyika na kwa mujibu wa sheria zake misaada isiyo ya kiutu inastahili kusitishwa.
Msaada wa Marekani kwa Gabon haukuwa mkubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa Niger, nchi nyengine ya Afrika ambayo Marekani ilisimamisha utoaji wa msaada.
Wakuu wa jeshi wa gabon walimpindua Ali Bongo Ondimba mara tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi kufuatia uchaguzi uliokosolewa pakubwa kutokana na madai ya wizi wa kura.