1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Marekani yatahadharisha kuhusu hali mbaya ya hewa

23 Desemba 2022

Idara ya Hali ya Hewa ya Marekani imeonya kuhusu hali mbaya ya hewa katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4LMon
Weltspiegel 17.02.2021 | USA Mississippi | Wetter, Schnee
Picha: Barbara Gauntt/Clarion-Ledger/USA Today/REUTERS

Maafisa wamesema hali hiyo ya baridi kali inaweza kuhatarisha maisha.

Viwango vya joto vinatarajiwa kushuka hadi chini ya nyuzi 56 chini ya sifuri katika kipimo cha Celsius kwenye baadhi ya maeneo.

Kuanguka kwa theluji nyingi kunaweza kusababisha uharibifu wa miundombinu na kuvuruga ratiba za usafiri wakati huu wa sikukuu.

Kwa mujibu wa maafisa, hali hiyo mbaya ya hewa inaweza kusababisha joto kushuka kupita kiasi au hata vifo.

Maafisa wameelezea wasiwasi kwamba umeme unaweza kukatika kutokana na dhoruba na wamewataka watu kuahirisha safari.

Takribani safari 2,000 za ndege zilizopangwa jana na leo zimefutwa kutokana na hali mbaya ya hewa.