Marekani yatiwa wasiwasi na mashambulizi ya RSF
19 Oktoba 2023Matangazo
Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller, amesema nchi hiyo ina wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti kwamba kikosi cha wapiganaji cha RSF nchini Sudan wamezidishisha mashambulizi katika mikoa ya Darfur Kusini na Omdurman.
Soma zaidi: UN: Miezi sita ya mapigano nchini Sudan yasababisha vifo vya takriban watu 9,000
Mapigano kati ya Jeshi la Sudan na RSF yalizuka Aprili 15 kufuatia mzozo unaohusiana na mpango wa mpito kuelekea utawala wa kiraia, na yameuharibu mji mkuu wa Khaeroum na kusababisha mashambulizi yanayochochewa na ukabila katika eneo la Darfur.
Miller amesema Marekani imeitolea wito RSF kuacha mara kushambulia maeneo ya raia, na kuwalinda raia.