Marekani yatoa waranti kukamatwa kwa meli ya mafuta ya Iran
17 Agosti 2019
Wizara ya sheria inadai kuwa meli hiyo ni sehemu ya mpango "wa kufikia kinyume na sheria mfumo wa kifedha wa Marekani, kusaidia upelekaji kinyume na sheria mafuta nchini Syria kutoka Iran unaofanywa na jeshi la kulinda mapinduzi ya Kiislamu," ambayo Marekani imesema kuwa ni kundi la kigeni la kigaidi.
waranti huo unasema meli hiyo, ambayo bado imetia nanga katika eneo hilo linalo milikiwa na Uingereza la Gibraltar hadi jana Ijumaa, na mafuta yote yaliyomo katika meli hiyo yanalazimika kutaifishwa kwa misingi ya ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya nguvu za dharura za kiuchumi , pamoja na kukamatwa kwa kiasi cha dola 995,000 , katika akaunti ambayo haikutajwa katika benki moja nchini Marekani inayoshrikiana na kampuni ya biashara ya Paradise Global Trading LLC, ambayo imeiita kampuni ya Shell inayohusishwa na biashara ambayo inafanyakazi kwa niaba ya jeshi la Iran.
Hakuna taarifa za haraka kutoka Uingereza ama Gibraltar kuhusiana na iwapo watachukua hatua kuhusiana na waranti huo, wakati Iran imesema inatuma wafanyakazi wengine wapya kuiendesha meli hiyo pamoja na shehena yake xa mapipa milioni 2.1 ya mafuta.
Jaji akataa ombi la Marekani
Jaji alikataa hatua ya dakika za mwisho ya kisheria kutoka marekani ikidai kuwa meli hiyo ibakie imekamatwa. Kukamatwa kwa meli hiyo Julai 4 kumekuja huku kukiwa na hali ya wasi wasi mkubwa katika eneo la ghuba baada ya mashambulizi kadhaa yanayodaiwa kufanywa na Iran katika meli ndogo za mafuta.
Marekani ikieleza kuhusu kitisho cha Iran kwa washirika wa Marekani, ilipanua uwezo wake wa kijeshi katika eneo hilo kwa kupeleka meli mpya za kubebea silaha na ndege , makombora pamoja na ndege za ushambuliaji za mkakati.
Iran na Marekani zimekuwa zikivutana tangu pale rais wa Marekani Donald Trump alipoitoa nchi hiyo katika makubaliano muhimu ya kinyuklia mwaka 2015 baina ya mataifa makubwa yenye nguvu na Iran , na kurejesha vikwazo ambavyo vinaathari kubwa katika uchumi wa Iran.
Baada ya kukamatwa kwa meli ya Grace 1, Julai 19 Iran ilikamata meli yenye bendera ya Uingereza ya mafuta Stena Impero katika ujia wa bahari wa Hormuz.
Iran inasema meli hiyo ilikiuka "sheria za kimataifa za safari za baharini," lakini hatua hiyo inaonekana kwa kiasi kikubwa kuwa ni kulipiza kisasi kwa kukamatwa kwa Grace 1.