1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawawekea vikwazo wanamgambo washirika wa Uturuki

18 Agosti 2023

Marekani imeyawekea vikwazo makundi mawili ya wanamgambo yanayoungwa mkono na Uturuki na viongozi wao.

https://p.dw.com/p/4VJIs
Syrien US-Militär
Picha: Baderkhan Ahmad/AP/picture alliance

Marekani imewatuhumu wanamgambo hao kwa ukiukaji wa haki za binadamu huko kaskazi magharibi mwa Syria, eneo ambalo linadhibitwa na upinzani.

Vikundi hivyo ni kikosi cha Suleiman Shah na Kitengo cha Hamza pamoja na viongozi wake Mohammad Hussein al-Jasim, Walid Hussein al-Jasim, na Sayf Boulad Abu Bakr.

Kwa mfano kikosi cha Suleiman Shah kina tuhuma za utekaji nyara na unyang'anyi wa mali za wakazi, hasa wakazi wa Kikurdi wa Afrin, kuwalazimisha kukimbia makazi yao au kulipa fidia kubwa kwa kurejea kwenye mali zao au kwa familia.

Makundi hayo yanajiendesha katika mji wa Afrin, ambao umekuwa chini ya wapiganaji wa upinzani wanaoungwa mkono na Uturuki tangu 2018.