SiasaMali
Marekani yaweka vikwazo kwa baadhi ya maafisa wa Mali
25 Julai 2023Matangazo
Katika taarifa hapo jana, wizara ya fedha ya Marekani iliwawekea vikwazo waziri huyo, mkuu wa jeshi la anga, Alou Boi Diarra, na naibu wake, Adama Bagayoko, kwa kusaidia kuongezeka shughuli za kundi la Wagner nchini Mali .
Soma pia:HRW:Wanajeshi Mali,Wagner wamefanya mauaji ya raia kiholela
Brian E. Nelson, katibu wa wizara ya fedha anayehusika na masuala ya ugaidi na ujasusi wa kifedha, amesema maafisa hao wamewaweka watuwa nchi hiyo katika hatari ya kundi la Wagner na unyanyasaji wa haki za binaadamu huku wakitoa njia ya ufujaji wa rasilimali za nchi yao kwa manufaa ya shughuli za kundi hilo nchini Ukraine.