1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marufuku ya usalama nchini Burkina Faso kuisha leo

27 Desemba 2021

Marufuku ya kutotoka nje usiku iliyowekwa mnamo Oktoba katika mkoa wa Mashariki wa Burkina Faso inafika mwisho leo. Amri ya kutotoka nje ilitolewa ili kupunguza mashambulizi ya makundi ya wapiganaji.

https://p.dw.com/p/44re3
Burkina Faso Gorgadji | Soldaten auf Patroullie
Wanajeshi wa Burkina Faso wakipiga doria kwenye barabara ya GorgadjiPicha: LUC GNAGO/Reuters

Wiki iliyopita, watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo waliwaua takriban wapiganaji 41 wa kundi la wapiganaji wa kujitolea la Homeland Defence linaloungwa mkono na serikali katika mashambulizi katika mkoa wa Kaskazini wa Loroum.

Serikali ilitangaza siku mbili za maombolezo ya wahanga hao.

Kuongezeka kwa ghasia za wanamgambo hao kumechochea wito wa upinzani wa kumtaka Rais Roch Marc Kabore ajiuzulu.

Wanamgambo wanaohusishwa na makundi ya al-Qaeda na lile linalojiita dola la kiislamu IS wamelaumiwa kwa mashambulizi mengi mabaya na utekaji nyara kaskazini na mashariki mwa Burkina Faso tangu 2015.