1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashabiki waonyesha kutoridhishwa na mashindano ya AFCON

13 Januari 2022

Mashabiki wa soka barani Afrika wameonyesha kutoridishwa na matukio yanayoshuhudiwa kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON yanayoendelea nchini Cameroon, huku baadhi wakisema matukio hayo yanaonyesha wazi kwamba kulikuwepo na matayarisho duni na huenda soka la Afrika likatiwa doa.

https://p.dw.com/p/45Ulo

Katika tukio la kushangaza katika mechi ya Jumatano kati ya Tunisia na Mali, refarii Janny Sikazwe alipuliza kipenga cha mwisho kunako dakika ya 85 ya mwisho na kuibua hasira miongoni mwa wachezaji na benchi la kiufundi la Tunisia. Je, hali hii inatishia kuondoa ladha ya mashindano hayo makubwa zaidi barani Afrika? Babu Abdalla amezungumza na mchambuzi wa michezo kutokan nchini Kenya, Hassan Ali Kauelni na kwanza alitaka kufahamu zaidi iwapo kwa upande wake ameridishwa na viwango vya urefarii hadi sasa.