1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbatia apingana na Nyambabe, Mosore

Mohammed Khelef25 Septemba 2015

NCCR-Mageuzi, ambacho ni moja ya vyama vinavyounda muungano wa upinzani wa UKAWA nchini Tanzania, imekanusha taarifa zilizotolewa na makamu mwenyekiti na katibu mkuu wake ya kutofuatwa katiba yake.

https://p.dw.com/p/1GdRb
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.Picha: DW/M.Khelef

Haya yanajiri siku moja baada ya Katibu Mkuu wake, John Mosena Nyambabe, na Makamu Mwenyekiti, Letisia Ghati Mosore, kufanya mkutano na waandishi wa habari na kudai kuwa chama chao hakinufaiki na UKAWA na badala yake CHADEMA ndio inayonufaika zaidi na kumtaka mwenyekiti wao, James Mbatia, kuitisha haraka mkutano wa kichama ili kujadili hali hiyo. Sikiliza ripoti ya Hawa Bihoga kutoka Dar es Salaam.