1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulio ya Istanbul yalaumiwa vikali kimataifa

16 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CG0a

JERUSALEM/BERLIN: Baada ya kushambuliwa mahekalu mawili ya Kiyahudi nchini Uturuki, Israel imetoa mwito wa kimataifa wa kuweko ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na uovu kama huo. Mwenye Kiti wa Baraza la Mawaziri wa Nje la UU, Franco Frattini wa Uitalia, aliiahidi Uturuki misaada ya kiutu ya UU. Na mjini Berlin serikali ya Ujerumani ilisema imetikiswa sana na mashambulio hayo. Kansela Gerhard Schröder amempelekea Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Erdogan risala ya kusisitiza masikitiko yake makubwa kwa maafa hayo. Naye Waziri wa Mambo ya Nje, Joschka Fischer alisema mashambulio hayo yanayonesha umuhimu wa kuweko ushirikiano wa kimataifa katika kupigana na ugaidi wa kimataifa na chuki dhidi ya Wayahudi. Katibu Mkuu wa Shirika la Kujihami la Magharibi, NATO, George Robertson aliyaita hayo mashambulio ya kinyama kabisa ya kuuawa watu wasioahusika. Pia Rais wa Marekani George W. Bush ameyalaumu vikaoli mashambulio hayo ya Istanbul.