1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi DR Congo yaua wanajeshi 2 wa Afrika Kusini

27 Juni 2024

Mashambulizi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha vifo vya wanajeshi wawili wa Afrika Kusini na kuwajeruhi wengine 20, hii ikiwa ni kulingana na jeshi Jumatano.

https://p.dw.com/p/4hawH
Afrika Kusini ilipeleka wanajeshi 2,900 mashariki mwa Kongo katikati mwa Disemba, 2023.
Afrika Kusini ilipeleka wanajeshi 2,900 mashariki mwa Kongo katikati mwa Disemba, 2023.Picha: picture alliance / Xinhua News Agency

Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini lilisema moja ya kambi zake ilishambuliwa siku ya Jumanne katika mji wa Sake, ulioko kilomita 25 magharibi mwa Goma katika jimbo lenye utulivu la Kivu Kaskazini. 

Jeshi hilo limesema wanajeshi wake wanne waliojeruhiwa vibaya wamelazwa hospitalini, huku wengine waliopata majeraha madogo wakitarajiwa kuruhusiwa hivi karibuni.

Afrika Kusini ilipeleka wanajeshi 2,900 mashariki mwa Kongo katikati mwa Disemba.

Wanajeshi hao ni sehemu ya kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC, wanaioisaidia serikali kukomesha uasi.