1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi Idlib yaweka mbinyo makubalino ya Uturuki na EU

Sekione Kitojo
29 Desemba 2019

Mashambulizi katika jimbo la Idlib nchini Syria yanasababisha maelfu ya raia kukimbia, wengi wao kwenda Uturuki.

https://p.dw.com/p/3VRvA
Syrien Flucht aus Idlib Provinz
Picha: picture-alliance/AA/M.B. Karacaoglu

Rais wa  Uturuki Tayyip Erdogan ameonya kuwa makubaliano kuhusu wakimbizi na  Umoja  wa  Ulaya  yamo hatarini.

Kwa wiki  kadhaa jimbo  la  Idlib nchini  Syria , ngome  ya  mwisho iliyobaki ya  waasi  wa  jihadi , limekuwa  likishambuliwa  kutoka majeshi  ya  serikali  ya  Syria na  Urusi. Mashambulizi  ya makombora , maroketi na  mashambulizi  ya  angani  yamesababisha miji  mingi kuharibika. Kutokana  na  mashambulizi  yanayoendelea , chama  cha  madaktari  wa  Marekani (SAMS), shirika  linalotoa msaada  wa  matibabu, limefunga  operesheni  zake  katika  hospitali mbili za  jimbo  hilo.

Syrien Idlib | Menschen auf dem Weg zur türkischen Grenze
Msafara wa wakimbizi kutoka Syria wakikimbilia UturukiPicha: picture-alliance/AA/E. Musa

Shirika  la  Medico International , shirika  la  kutoa  misaada ya  kiutu pamoja  na  haki  za  binadamu, limeripoti kuwa  katika  muda  wa wiki  kadha zilizopita , kiasi  cha  hospitali 100 zimeshambuliwa  kwa makusudi  kwa  mabomu.

Kutokana  na  mashambulizi  haya  yanayoendelea, mamia  kwa maelfu ya  raia  wamekimbia  makaazi  yao . Kwa  mujibu wa  kundi la urtibu la  kuchukua  hatua  za kutoa  misaada, kiasi  ya  watu 217,000 wamekimbia  tangu Novemba mwaka  huu.

Rais  wa  Uturuki Recep Tayyip Erdogan  ameonya  kuwa  hatua mpya  ya  watu  kukimbilia  nchini  humo  kwa  wingi , kama ilivyokuwa  mwaka  2015, wakati  idadi  kubwa  ya  walioomba hifadhi  waliingia  katika  mataifa  ya  Ulaya , huenda  ikatokea.

Syrien Idlib | Syrier in Harbanos
Wengi hawana uchaguzi ila kukimbia mashambulizi ya jeshi la Syria na Urusi katika jimbo la IdlibPicha: picture-alliance/AA/M. Said

Mamia wakimbia  mashambulizi Syria

Amesema  kampeni ya  mashambulizi  katika  jimbo  la  Idlib tayari imesababisha  watu 80,000  kukimbia  kutoka  jimbo  hilo, ambao sasa  wanaelekea  Uturuki. Rais amesema  nchi  yake " haiwezi tena  kubeba mzigo  huo yenyewe," na  kuongeza  kuwa "Nchi  zote za  Ulaya , na  hususan Ugiriki, zitakuja  kupata  athari zake" kutokana  na  watu  wengi  kukimbia  nchi  hiyo.

makubaliano  na  Umoja  wa  Ulaya  yanaitaka  Uturuki  kuzuwia waomba  hifadhi  kuondoka  kutoka  katika  ardhi  yake  kwenda katika  visiwa  vya  karibu  vya  Ugiriki  kwa  msaada  wa  watu wanaosafirisha  watu  kwa  njia  haramu. Kwa  upande  wake  Uturuki , hadi  mwaka  uliopita  itapata  kutoka  Umoja  wa  Ulaya  euro bilioni 6 kuimarisha  hali  ya  maisha  ya  wakimbizi  waliokimbilia  Uturuki.

Makubaliano  hayo  pia  yanalenga  kuwa  wahamiaji  ambao hawana  hadhi ya  ukimbizi  barani  Ulaya  watarejeshwa  kutoka visiwa  vya  Ugiriki kwenda  uturuki.

Syrien, Idlib: Erneute Zerstörung und Flucht
mashambulizi ya jeshi la Syria katika mji wa Maaret al-Numan katika jimbo la idlib nchini SyriaPicha: Getty Images/AFP/A. Ketaz

Umoja  wa  Ulaya  pia  umeahidi  kuanza  mazungumzo  juu ya kuondoa mahitaji  ya  visa  kwa  raia  wa  Uturuki  kwenda  Ulaya na  uwezekano  wa  Uturuki  kuwa  mwanachama  wa  Umoja  huo.

Uturuki  kwa  sasa , inataka  kujadili  makubaliano  yaliyopo hivi sasa  kutokana  na  kuongezeka  kwa  idadi  ya  wakimbizi. Na mapema  majira  ya  joto  mwaka  huu, Erdogan  alitishia kuwaruhusu waomba  hifadhi  kusafiri  kwenda  Ulaya  hadi  pale Umoja  huo  utakapoongeza  msaada  wake  wa  kifedha  kwa wakimbizi  wanaoishi  Uturuki. Hadi  sasa  Uturuki  imewachukua wakimbizi wapatao  milioni 3.6  kutoka  Syria.