1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya makombora katika miji kadhaa ya Ukraine

10 Oktoba 2022

Shambulizi la makombora la Urusi limeharibu majengo ya makazi ya watu katika mji wa Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine na kuuwa watu 12.

https://p.dw.com/p/4Hz4r
Ukraine Krieg mit Russland Raketen auf Kiew
Picha: Adam Schreck/AP Photo/picture alliance

Mashambulizi ya makombora katika miji ya Ukraine ukiwemo mji mkuu wa Kyiv, yamesababisha vifo vya watu kadhaa na wengine kujeruhiwa leo Jumatatu, ikiwa ni siku moja baada ya Moscow kuishutumu Kyiv kwa mlipuko uliotokea kwenye daraja linalounganisha Crimea na Urusi. Kyrylo Tymoshenko, Naibu mkuu wa ofisi ya rais, ametoa wito kwa wakaazi katika miji ambayo imekumbwa na mashambulizi kusalia majumbani na kuongeza kwamba Ukraine ipo chini ya mashambulizi ya makombora. Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko amethibitisha kutokea kwa mashambulizi hayo alioyataja kufanywa na Urusi. Video zilizowejwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha moshi mweusi ukitanda angani kwenye maeneo kadhaa ya jijini hilo. Rais Volodymyr Zelensky ameituhumu Urusi akisema azma ya Moscow ni kuifuta Ukraine kwenye ramani ya dunia.