1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya Israel yawaua watu 26 wakiwemo polisi Gaza

Sylvia Mwehozi
3 Januari 2025

Mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu wasiopungua 26 katika Ukanda wa Gaza, wakiwemo maafisa wawili wa ngazi ya juu katika jeshi la polisi linaloongozwa na Hamas.

https://p.dw.com/p/4omED
Gaza | Jabaliya | Shambulizi la Israel
Gaza | Jabaliya | Shambulizi la IsraelPicha: Mohammed Alaswad/AP

Mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu wasiopungua 26 katika Ukanda wa Gaza, wakiwemo maafisa wawili wa ngazi ya juu katika jeshi la polisi linaloongozwa na Hamas. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa maafisa wa Palestina na hospitali.

Mashambulizi hayo yalilenga eneo la kibinadamu lililotangazwa na Israel na kusababisha vifo vya watu 11wakiwemo watoto watatu. Watu wengine wameuawa katika mashambulizi yaliyotokea katika mji wa kusini wa Khan Younis na katika kambi ya wakimbizi ya Maghazi katikati mwa Gaza.

Wizara ya mambo ya ndani inayoongozwa na Hamas imelaani mauaji hayo ikisema kwamba maafisa hao wawili wa polisi walikuwa wakitekeleza wajibu wao wa kibinadamu na kitaifa katika kuwahudumia Wapalestina. Israel ilisema mashambulizi hayo yalilenga mwanachama mwandamizi wa vyombo vya usalama vya ndani vya Hamas.