Mashambulizi ya kigaidi mjini Barcelona ni unyama
21 Agosti 2017Inaelekea kukaribia kufikia mwisho kwa kundi linalojiita Dola la Kiislamu hatari ya mashambulio ya kigaidi inaongezeka, kwa kuwa wapiganaji wa kundi hilo hataki tena kurejea upande wa kusini. Inatia hofu kwamba mbinyo dhidi ya kundi la Waislamu wenye itikadi kali wanapanga kuwaingiza washambuliaji wao katika mataifa ya magharibi, ili kulipiza kisasi cha kushindwa kwao. Jumuiya ya kimataifa , licha ya mafanikio yaliyopatikana, dhidi ya kitisho cha kundi la Dola la Kiislamu , inahitaji pamoja na hayo, kujihakikishia ulinzi imara, pamoja na kubakia katika msimamo wetu wa kidini na kulinda maadili yetu kwa pamoja. Kwa kuwa mapambano dhidi ya ugaidi unaohusishwa na Mwenyezi Mungu , utaweza kushindwa tu kwa kutumia nguvu za dola na sio kwa kutumia hali ya maridhiano yasiyo sahihi.
Gazeti la Lausitzer Rundschau kutoka mjini Cottbus likizungumzia kuhusu shambulio la kigaidi nchini Uhispania , linaandika.
Jibu litakalokuwa mjarabu kabisa kwa tukio kama hilo la Uhispania , kutokana na mauaji hayo ya kuchukiza na wendawazimu waliohusika katika mauaji hayo, ni pale mtu atakapojizuwia kubadili maisha yake ya msingi, licha ya ugaidi huo. Washambuliaji kwa upande wao wanaonesha chuki tu na matumizi ya kinyama ya nguvu, zaidi ya hayo hakuna. Ilikuwa jambo zuri, kwamba wagombea katika uchaguzi siku ya Ijumaa walipounguza shughuli zao na kutoa ishara ya umoja. Tukio la kigaidi pamoja na maombolezi ya wahanga havikutumika , kwa ajili ya kujipatia umaarufu usiostahili katika uchaguzi wa Ujerumani. Hali hii inaonesha ukomavu wa demokrasia. Sio kwamba , katika mapambano ya kuwania madaraka katika uchaguzi , suala la ulinzi zaidi lisizungumziwe, la , ni kunyume chake.
Kwa upande wa kuondolewa kwa mshauri mkuu wa mikakati kwa rais Donald Trump wa Marekani katika Ikulu ya Marekani ya White House Stephen Bannon , gazeti la Fränkischer Tag la mjini Bamberg linaandika.
Kwa rais kutotaja kwa jina lake sahihi wanazi mamboleo , na kuanza kujificha katika uongo, kila kitu hapa kinaonekana kuwamo katika mikono ya Bannon. Akiwa ni mwenye msimamo mkali na anayetoka katika jarida la habari la msimamo mkali wa mrengo wa kulia la Breitbart, sumu ya Bannon ataisambazwa zaidi hapo baadaye kwa kiwango kikubwa. Pamoja na kudhibitiwa kutoka Ikulu ya Marekani ya White House , lakini hakuna mtu mwingine anayeweza kushindana nae.
Gazeti la Südwest-Presse la mjini Ulm linazungumzia kuhusu mjadala unaoendelea nchini Ujerumani kuhusiana na kuweka ukomo wa kuruhusu wakimbizi kuingia nchini humo. Gazeti linaandika.
Isisahaulike kwamba , bila ya kuwekwa ukomo wa kuruhusu wakimbizi kuingia nchini humu, hakutakuwa na makubaliano ya muungano wa kuunda serikali. Kusahau litakuwa pigo kwa kansela katika mkutano mkuu wa chama ndugu na chama cha kansela cha CSU. Hali ilivyo sasa ni kwamba ukomo huo umekwisha fikiwa. Je mzigo huo sasa umewekwa kando ? Ni kawaida ya vyama hivyo ndungu , kwamba katika wakati wa kampeni ushindi uwe umehakikishwa kwa kuondoa kila kinachoweza kuzuwia , ikiwa ni pamoja na mizozo, kinyume na upande wa chama kikuu cha upinzani cha SPD , hali hiyo haraka imefichwa chini ya zulia. Njia hiyo haiondoi uchafu. katika majadiliano ya kuunda muungano wa serikali suala la ukomo litajitokeza bila shaka.
Msimu mpya wa ligi ya Ujerumani Bundesliga, umeanza rasmi , linaandika gazeti la Badische Neueste Nachrichten la mjini Karlsruhe. Mhariri anaandika.
Mpira katika Bundesliga umeanza kudunda tena, na hii ni katika msimu wa 55. Mafanikio ya kandanda la Ujerumani tayari yanaangaliwa tena. Kuanzishwa kwa ushahidi wa kutumia vidio una maana ya uamuzi wa haraka katika historia ya ligi hiyo, kuweza kujua iwapo kila kitu kinakwenda sahihi , ama la.
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman